Reports from the Maasai community of Loliondo in Ngorongoro District, Tanzania, indicate that people are being forcefully evicted from their ancestral lands and territories, starting on 10 June 2022. The ICCA Consortium strongly condemns this inexcusable violence against the Indigenous Maasai
First published on 06/12/2022, and last updated on 08/08/2023
Warning: This alert includes disturbing content about human rights violations and violence against Indigenous Peoples. Note: This alert was updated with new and additional information on 6 July 2022.
Friday 10 June was a dark day for the Maasai of Loliondo following the forceful evictions of the community from their lands, reportedly to create a game reserve for wealthy foreign hunters. After months of threats, tensions have been particularly high since 7 June, when an estimated 700 troops (including police, park rangers, military and other security forces) arrived in Loliondo and invaded their territories by starting to demarcate 1500 km2 in preparation for evictions to create a game reserve. Thousands of Maasai protested this escalation in defense of their ancestral rights to the lands.
Download: Media advisory for immediate release
“The violent eviction of the Maasai community in Loliondo, Tanzania” (PDF File)
Reports by media, civil society organizations and political parties in Tanzania show the graphic events and injuries sustained by members of the Maasai community. Videos shared on public social media platforms show people fleeing the terrifying evictions, gunshots and smoke rising in the distance, reportedly from tear gas thrown at people. At the time of publication on 12 June, grassroots organizations operating in the area have identified at least 31 people seriously injured by the security forces and admitted to various hospitals across the border in Kenya. A police officer was also reportedly killed in the conflict.
Information continues to be gathered about how many people have been affected and harmed. Accurate reporting is hindered by the government of Tanzania’s intimidation of journalists, lawyers and civil society organizations and suppression of freedom of speech and independent media.
There is no context in which such violence against Indigenous Peoples can be allowed or accepted, including in the name of conservation. It must not be tolerated and the perpetrators must be held accountable.
In February 2022, the Maasai of Loliondo called out for support through a petition to the government of Tanzania following the latest round of threats of evictions from their lands, purportedly to create a game reserve to be controlled by the Ortello Business Corporation, which runs hunting excursions for the United Arab Emirates’ royal family and guests. According to the Oakland Institute, the influence of this company has led to previous violations of the Maasai communities’ rights through evictions, burning of homes and killing of livestock. On 25 May 2022, communities also submitted a comprehensive report on the best way the land in question should be used to the Tanzanian Prime Minister, with no response or any rounds of meaningful discussion.
It is clear that the government of Tanzania has not properly considered or responded to the communities’ calls to drop these eviction plans, which were amplified by more than three million supporters across the world.
“Why are Tanzania’s Maasai being forced off their ancestral land?”
28 February 2022 episode of The Stream, Al Jazeera.
The ICCA Consortium condemns the continued use of fortress conservation and the cycle of violence perpetrated against the Maasai through decades of threats, exclusion and evictions from their ancestral lands in northern Tanzania.
We stand in solidarity with the Maasai of Loliondo who are resisting these threats and violations and urge the government of Tanzania to:
- Immediately halt the violent evictions of the Maasai and withdraw all paramilitary and armed forces from their ancestral lands;
- Bring to an end the brutal mistreatment, injuries and suffering caused by the evictions, shootings and intimidation and bring to justice the perpetrators of this violence, including the intellectual authors and financiers;
- Ensure the affected community members have emergency and ongoing access to adequate and culturally appropriate health care and psychosocial support;
- Allow journalists, human rights observers, lawyers and civil society organizations to access Loliondo, speak with affected Maasai pastoralists and report on the situation freely and without intimidation, harassment or coercion;
- Respond to the communities’ report submitted to the Prime Minister on 25 May 2022, which includes their views on how the land in question should be used;
- Uphold commitments to protect human rights, including the rights of Indigenous Peoples, and to appropriately recognize and support conservation by Indigenous Peoples and local communities under the UN Convention on Biological Diversity; and
- Refrain from over-reliance on foreign investors and commit to locally rooted, equitable approaches to conservation of the Loliondo area in partnership with the Indigenous Peoples of Tanzania, for example, by supporting the Maasai to secure legal rights through Certificates of Customary Right of Occupancy.
We call upon conservation organizations and funders as well as tourism operators and individual tourists who are supporting or seeking to support conservation initiatives in Tanzania to take a clear stand against this violence and back the self-determined priorities of the Maasai – the original conservationists of the Ngorongoro and Serengeti.
We also call on the general public to take action in support of the Maasai by signing this online petition via Avaaz and sharing it with friends and networks. Add your voice to the more than three million people who have already signed it (at the time of publication) and help meet the Ngorongoro leaders’ goal of 3.5 million supporters.
UPDATES
As of 6 July 2022, the situation in Loliondo continues to be incredibly tense. The Government of Tanzania has gone to great lengths to deny any wrongdoing and has clamped down on independent media coverage and civil society organisations within the country. However, the evictions have been the subject of extensive independent reporting and sparked international outcry and widespread condemnation (see links below).
In addition to the dozens of people injured by live ammunition, tear gas and beatings and hundreds forced to flee armed units on 10 June 2022, the 1500 km2 of village land was reportedly gazetted as a Game Controlled Area on 17 June without following the necessary legal procedures and in contravention of international law. According to a press release published by the Ministry of Natural Resources and Tourism, the demarcation of the 1500 km2 “…as a reserved area for conservation [is] for the benefit of the present and future generations not only for the United Republic of Tanzania but also for the rest of the world.”
International biodiversity law and conservation policy are clear that protected and conserved areas cannot be established through violations of human rights. The ICCA Consortium strongly condemns the invocation of “conservation” as a thinly veiled justification for the widespread violence. Even international conservation organisations have questioned whether the plans for the area can legitimately be considered as intended for “conservation” purposes, when the national government appears to be primarily motivated by economic opportunities of foreign investment and hunting operations.
In late June in Nairobi, during the fourth round of negotiations on the post-2020 global biodiversity framework, Maasai community members from Loliondo presented a statement on the evictions, saying:
“Our homeland has been turned into a hunting park, with wealthy people coming in to hunt the wildlife. We have witnessed this killing of wildlife for fun since 1992, when the royal family from Dubai was given an open-ended license to our village lands. The guns are now turned to us – the very people who have taken care of the environment and shared harmony, food, and peace with wildlife for time immemorial. Hunting and conservation do not go together, but with the power of money, anything is seemingly possible.”
LISTEN: “In Tanzania, the Maasai may lose their land – again” (Al Jazeera Podcast, The Take, 11 July 2022)
We have received the following information concerning the continued government crackdown on and legal harassment and intimidation of the Maasai communities in Loliondo, Ngorongoro District (current as of 6 July 2022):
- A total of 25 Maasai leaders, including ward councilors and the District Chairman of the ruling party (CCM), have now been charged with conspiracy to commit murder and causing the death of the police officer on 10 June. Their court case was initially scheduled for 30 June but has been postponed to 14 July. Lawyers and family members have asked for the case to be fast-tracked because some of the accused are very elderly.
- New reports indicate that there is a growing number of people arrested, charged with murder, and held in custody at Kisongo prison. At the time of publication, 27 people are waiting to be sent to court on 14 July.
- Security forces continue to forcefully evict people and livestock from demarcated land for the designated Game Reserve in Loliondo. Livestock found within the demarcated area has been taken and locked up and families looking for their livestock have been asked for large sums of money to get their livestock back.
- After the government called for a crackdown on “illegal immigrants”, over 72 community members in Loliondo have been arrested and accused of being Kenyans. With the support of lawyers representing them at the district court, most of them were released after they were confirmed as Tanzanian citizens, but some remain detained for unknown reasons and durations.
INDEPENDENT MEDIA COVERAGE
Since this alert was first published on 12 June 2022, the evictions in Loliondo have been the subject of extensive independent reporting, including the following:
- “Tension in Tanzania’s Loliondo area as troops move in to evict the Maasai” – Nation, 12 June 2022
- “Maasai protesters shot, beaten as Tanzania moves forward with wildlife game reserve” – Mongabay, 14 June 2022
- “Maasai leaders arrested in protests over Tanzanian game reserve” – The Guardian, 14 June 2022
- “Rights groups condemn Tanzanian police violence against Maasai” – Al Jazeera, 15 June 2022
- “Tanzania: More violence feared over bid to evict Maasai from ancestral lands” – UN News, 15 June 2022
- “Focus on Africa – Tanzania’s Maasai evictions continue” – BBC Sounds, 15 June 2022
- “Tanzania starts moving Maasai out of Ngorongoro reserve” – France24/AFP, 16 June 2022)
- “Violent clashes as Masai ‘driven off land’ for Emirati trophy hunters” – The Times, 18 June 2022
- “Mzozo wa Loliondo: Miaka 30 ya machungu na matumaini” (“Loliondo Conflict: 30 Years of Pain and Hope”) – BBC News Swahili, 18 June 2022
- “Loliondo clashes: The Maasai seeking medical help in Kenya” – BBC News, 21 June 2022
ORGANISATIONAL AND OTHER STATEMENTS
The evictions in Loliondo sparked an international outcry and widespread condemnation. A wide range of UN experts, human rights and land rights organisations, conservation organisations, academic institutions and researchers, and notable individuals have issued statements, including:
- African Commission on Human and Peoples’ Rights: “Urgent call for cessation of the eviction of the Maasai community in the Ngorongoro district in The United Republic of Tanzania” (13 June 2022)
- UN Permanent Forum on Indigenous Issues: “Statement by the Chairperson of the Permanent Forum on the eviction of Maasai people from the Ngorongoro Conservation Area in Tanzania” (14 June 2022)
- UN Special Rapporteurs: “Tanzania: UN experts warn of escalating violence amidst plans to forcibly evict Maasai from ancestral lands” (15 June 2022)
- Oakland Institute: “URGENT ALERT – Heavy Police Presence in Loliondo as Threats of Mass Evictions of the Maasai Intensify” (9 June 2022)
- Forest Peoples Programme (ICCA Consortium Member): “Press Release: “We will not leave. Not now. Not ever”: Tanzanian state violently seizes Maasai land in Loliondo” (13 June 2022)
- International Work Group for Indigenous Affairs (IWGIA): “Urgent Alert: New serious threats towards the Maasai people of Loliondo in Tanzania” (13 June 2022) and “Situation of Maasai in Loliondo and Sale in Tanzania dangerous and desperate” (05 July 2022)
- Amnesty International: “Tanzania: Halt brutal security operation in Loliondo” (15 June 2022)
- International Land Coalition: “Maasai being forcefully evicted from their lands” (15 June 2022)
- Frankfurt Zoological Society: “Appraisal of the situation of Loliondo” (11 June 2022)
- International Union for Conservation of Nature (IUCN): “IUCN Statement on human rights violations in Loliondo, Tanzania” (19 June 2022) and “Statement on human rights abuses in conservation” (28 June 2022)
- Conservation International: “Conservation International Statement on Reports of Violence Against Indigenous Peoples in Tanzania” (24 June 2022)
- Open letter: “Violation of African Union and United Nations Standards on Land Governance” – by the University of the Western Cape, Institute for Poverty, Land and Agrarian Studies (16 June 2022)
- Opinion article: “East Africa must reject its colonial model of conserving wildlife” – by author and freelance journalist Gatu wa Mbaria, published by the Guardian (24 June 2022)
- Opinion article: “Loliondo evictions: bad for people, conservation and pastoralism” – by researchers Lucas Yamat and Pablo Manzano, published by Pastres (24 June 2022)
- Open letter: “Open letter to Her Excellency President Samia Suluhu Hassan regarding Loliondo and Ngorongoro saga” – by Professor Emeritus Issa G. Shivji, School of Law, University of Dar Es Salaam (25 June 2022)
LEARN MORE
Kiswahili / Swahili
Tahadhari: Wamaasai Nchini Tanzania Wanafukuzwa Kwa Nguvu Kutoka Kwenye Ardhi Ya Mababu Zao
Onyo: Tahadhari hii inajumuisha maudhui ya kusikitisha kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu na unyanyasaji dhidi ya watu wa asili. Kumbuka: Taarifa hii ilisasishwa kwa maelezo mapya na ya ziada mnamo tarehe 6 Julai 2022.
Ijumaa ya tarehe 10 Juni ilikuwa siku ya giza kwa Wamaasai wa Loliondo kufuatia jamii hiyo kufukuzwa kwa nguvu kutoka katika maeneo yao, ikidaiwa kuwa ni eneo la hifadhi kwa ajili ya wawindaji matajiri wa kigeni. Baada ya vitisho vya miezi kadhaa, hali ya wasiwasi imekuwa kubwa hasa tangu tarehe 7 Juni, ambapo angalau askari 700 (wakiwemo polisi, askari wa hifadhi, wanajeshi na vikosi vingine vya ulinzi na usalama) walifika Loliondo na kuvamia maeneo yao kwa kuanza kutenga eneo la kilomita mraba 1500 kwa ajili ya maandalizi ya kuwaondoa kwa minajili ya kuunda hifadhi ya wanyamapori. Maelfu ya Wamaasai walipinga ongezeko hili wakitetea haki za mababu zao kwa ardhi.
Pakua: Ushauri wa Vyombo vya Habari wa Kutolewa Haraka
“Kufukuzwa kwa vurugu kwa jamii ya Wamaasai huko Loliondo, Tanzania” (PDF)
Ripoti za vyombo vya habari, asasi za kiraia na vyama vya siasa nchini Tanzania zinaonyesha matukio na majeraha waliyopata watu wa jamii ya Kimaasai. Video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakikimbia kufukuzwa kwa kutishwa, milio ya risasi na moshi ukipanda kwa mbali, kutokana na kurushwa kwa mabomu ya machozi. Wakati wa kuchapishwa tarehe 12 Juni, mashirika ya vijijini yanayofanya kazi katika eneo hilo yamegundua angalau watu 31 waliojeuriwa vibaya na vikosi vya usalama na kulazwa katika hospitali mbali mbali za mpaka wa Kenya. Afisa wa polisi pia aliripotiwa kuuawa katika mzozo huo.
Taarifa zinaendelea kukusanywa kuhusu watu wangapi wameathirika na kudhurika. Utoaji wa taarifa sahihi unazuiwa na vitisho vya serikali ya Tanzania dhidi ya waandishi wa habari, wanasheria na asasi za kiraia na kuminya uhuru wa kujieleza na vyombo huru vya habari.
Hakuna muktadha ambapo unyanyasaji kama huo dhidi ya Wenyeji unaweza kuruhusiwa au kukubalika, ikijumuisha kwa jina la uhifadhi. Ni lazima isivumiliwe na wahusika wawajibishwe.
Mnamo Februari 2022, Wamasai wa Loliondo waliomba kuungwa mkono kupitia ombilao kwa serikali ya Tanzania kufuatia vitisho vya hivi karibuni vya kufukuzwa katika maeneo yao, kwa madai ya kuunda pori litakalodhibitiwa na Kampuni ya Biashara la Ortello, linaloendesha uwindaji. Safari za familia ya kifalme ya Falme za Kiarabu na wageni. Kulingana na Taasisi ya Oakland, ushawishi wa kampuni hii umesababisha ukiukaji wa awali wa haki za jamii za Wamaasai kupitia kufukuzwa, kuchoma manyumba na kuua mifugo. Tarehe 25 Mei 2022, jumuiya pia ziliwasilisha ripoti kuhusu njia bora ya ardhi inayohusika itumike kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, bila majibu au mijadala yoyote ya maana.
Ni wazi kuwa serikali ya Tanzania haijazingatia ipasavyo au kuitikia wito wa jumuiya wa kuachana na mpango huu wa kuwahamisha watu, ambao iliongezewa nguvu na wafuasi zaidi ya milioni tatu duniani kote.
]Kwa nini Wamaasai wa Tanzania wanalazimishwa kuondoka kwenye ardhi ya mababu zao?”
Tarehe 28 Februari 2022 kipindi cha The Stream, Al Jazeera.
ICCA Consortium inalaani kuendelea kwa uhifadhi wa ngome na mzunguko wa ukatili unaofanywa dhidi ya Wamaasai kupitia miongo kadhaa ya vitisho, kutengwa na kufukuzwa kutoka kwa ardhi ya mababu zao kaskazini mwa Tanzania.
Tunasimama kwa mshikamano na Wamaasai wa Loliondo wanaopinga vitisho na ukiukaji huu na tunaitaka serikali ya Tanzania:
- Sitisha mara moja kufukuzwa kwa Wamaasai kwa jeuri na kuwaondoa wanajeshi na wanajeshi wote katika ardhi ya mababu zao;
- Komesha unyanyasaji wa kikatili, majeraha na mateso yanayosababishwa na kufukuzwa, kupigwa risasi na vitisho na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahusika wa vurugu hizi, wakiwemo waandishi wasomi na wafadhili;
- Hakikisha wanajamii walioathirika wanapata huduma ya dharura na inayoendelea ya huduma za afya zinazofaa na zinazofaa kitamaduni na msaada wa kisaikolojia;
- Ruhusu waandishi wa habari, waangalizi wa haki za binadamu, wanasheria na asasi za kiraia kufika Loliondo, kuzungumza na wafugaji wa Kimasai walioathirika na kuripoti hali hiyo kwa uhuru na bila vitisho, manyanyaso au shuruti;
- Jibu ripoti ya jumuiya iliyowasilishwa kwa Waziri Mkuu tarehe 25 Mei 2022, ambayo inajumuisha maoni yao kuhusu jinsi ardhi inayohusika inapaswa kutumika;
- Timiza ahadi za kulinda haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na haki za Watu wa Kiasili, na kutambua na kuunga mkono ipasavyo uhifadhi wa Watu wa Asili na jumuiya za wenyeji chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Anuwai za Kibiolojia; na
- Jiupishe na utegemezi zaidi kwa wawekezaji wa kigeni na kujitolea kufuata misingi ya ndani, mbinu za usawa katika uhifadhi wa eneo la Loliondo kwa kushirikiana na Wenyeji wa Tanzania, kwa mfano, kuwaunga mkono Wamassai kupata haki za kisheria kupitia Hati za Haki ya Kimila ya Kumiliki.
Tunatoa wito kwa mashirika ya uhifadhi na wafadhili pamoja na waendeshaji utalii na watalii binafsi ambao wanaunga mkono au wanaotaka kusaidia mipango ya uhifadhi nchini Tanzania kuwa na msimamo wa wazi dhidi ya ukatili huu na kuunga mkono vipaumbele vya Wamaasai waliojiwekea wenyewe – wahifadhi asili wa Ngorongoro na Serengeti.
Pia tunatoa wito kwa umma kwa ujumla kuchukua hatua kuwaunga mkono Wamaasai kwa kusaini ombi hili la mtandaoni kupitia Avaaz na kuwashirikisha marafiki na mitandao. Ongeza sauti yako kwa zaidi ya watu milioni tatu ambao tayari wametia saini (wakati wa kuchapishwa) na usaidie kufikia lengo la viongozi wa Ngorongoro la wafuasi milioni 3.5.
SASISHO
Hadi tarehe 6 Julai 2022, hali ya Loliondo inaendelea kuwa ya wasiwasi mkubwa. Serikali ya Tanzania imekwenda mbali zaidi kukanusha makosa yoyote na imebana vyombo huru vya habari na asasi za kiraia ndani ya nchi. Hata hivyo, kufukuzwa kumekuwa mada ya kuripotiwa kwa kina huru na kuzua malalamiko ya kimataifa na kulaaniwa kwa wingi (tazama viungo hapa chini).
Mbali na makumi ya watu waliojeruhiwa kwa risasi za moto, mabomu ya machozi na kupigwa, na mamia kulazimika kukimbia askari waliokuwa na silaha tarehe 10 Juni 2022, eneo la kilomita mraba 1500 la ardhi ya kijiji lilivyotangazwa kwenye gazeti la serikali kama Eneo la Pori Tengefu mnamo Juni 17 bila kufuata sheria na taratibu zinazohitajika na kinyume na sheria za kimataifa. Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, kuwekewa mipaka ya kilomita mraba 1500 “…kama eneo lililotengwa kwa ajili ya uhifadhi [ni] kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho si kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee bali pia kwa dunia nzima.”
Sheria ya kimataifa ya bioanuwai na sera ya uhifadhi ziko wazi kwamba maeneo yaliyolindwa na yaliyohifadhiwa hayawezi kuanzishwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu. ICCA Consortium inalaani vikali ombi la “uhifadhi” kama uhalali uliofichwa kwa vurugu zilizoenea. Hata mashirika ya kimataifa ya uhifadhi yamehoji ikiwa mipango ya eneo hilo inaweza kuzingatiwa kihalali kama iliyokusudiwa kwa madhumuni ya “uhifadhi”, wakati serikali ya kitaifa inaonekana kuhamasishwa na fursa za kiuchumi za uwekezaji wa kigeni na shughuli za uwindaji.
Mwishoni mwa mwezi Juni in Nairobi, wakati wa duru ya nne ya majadiliano kuhusu mfumo wa bioanuwai wa kimataifa wa baada ya 2020, wanajamii wa Kimaasai kutoka Loliondo waliwasilisha taarifa kuhusu kufukuzwa kwao, wakisema:
“Ardhi ya makazi yetu imegeuzwa kuwa mbuga ya uwindaji, huku watu matajiri wakiingia kuwinda wanyamapori. Tumeshuhudia mauaji haya ya wanyamapori kwa kujifurahisha tangu 1992, wakati familia ya kifalme kutoka Dubai ilipopewa leseni isiyo na kikomo kwenye ardhi ya vijiji vyetu. Bunduki sasa zimegeuzwa kwetu – watu walewale ambao wametunza mazingira na kuishi kwa amani na kushirikiana chakula, na amani na wanyamapori tangu zamani. Uwindaji na uhifadhi haviendi pamoja, lakini kwa nguvu ya pesa, chochote kinawezekana.”
Sikiliza: “Nchini Tanzania, Wamaasai wanaweza kupoteza ardhi yao – tena” (Al Jazeera Podcast, The Take, 11 Julai 2022).
Tumepokea taarifa ifuatayo kuhusu msako wa serikalunaoende wa serikali dhidi ya kuwanyanyasa kisheria na kuwatishia wanajamii wa Kimasai huko Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro (sasa tarehe 6 Julai 2022):
- Jumla ya viongozi 25 wa Kimaasai wakiwemo madiwani wa kata na Mwenyekiti wa chama tawala (CCM) Wilaya sasa wameshtakiwa mahakamani kwa tuhuma za kula njama za mauaji na kusababisha kifo cha askari polisi huyo tarehe 10 Juni. Kesi yao mahakamani hapo awali ilipangwa tarehe 30 Juni lakini imeahirishwa hadi Julai 14. Mawakili na wanafamilia wameomba kesi hiyo iharakishwe kwa sababu baadhi ya washtakiwa ni wazee sana.
- Taarifa mpya zinaonyesha kuwa kuna ongezeko la watu wanaokamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji na kuzuiliwa katika gereza la Kisongo. Wakati wa kuchapishwa, watu 27 wanasubiri kupelekwa kortini tarehe 14 Julai.
- Vikosi vya ulinzi na usalama vinaendelea kuwaondoa kwa nguvu watu na mifugo katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Pori Tengefu la Loliondo. Mifugo iliyokutwa ndani ya eneo lililotengwa imechukuliwa na kufungiwa na familia zinazotafuta mifugo yao zimeombwa kiasi kikubwa cha fedha ili kurejesha mifugo yao.
- Baada ya serikali kuitisha msako mkali dhidi ya “wahamiaji haramu”, zaidi ya wanajamii 72 huko Loliondo wamekamatwa na kushutumiwa kuwa Wakenya. Kwa msaada wa mawakili wanaowawakilisha katika mahakama ya wilaya, wengi wao waliachiliwa huru baada ya kuthibitika kuwa ni raia wa Tanzania, lakini baadhi yao wanaendelea kuzuiliwa kwa sababu zisizojulikana na muda.
Vyombo Huru vya Habari
Tangu tahadhari hii ilipochapishwa kwa mara ya kwanza tarehe 12 Juni 2022, suala la kufukuzwa Loliondo limepewa uzito na machapisho huru ya kina, zikiwemo zifuatazo:
- “Mvutano katika eneo la Loliondo nchini Tanzania huku wanajeshi wakiingia kuwaondoa Wamaasai” – Taifa, 12 Juni 2022.
- “Waandamanaji wa Kimaasai wapigwa risasi, kupigwa wakati Tanzania ikisonga mbele na pori la akiba” – Mongabay, 14 Juni 2022.
- “Viongozi wa Wamaasai wakamatwa katika maandamano ya kupinga hifadhi ya wanyama ya Tanzania” – The Guardian, 14 Juni 2022.
- “Makundi ya haki yalaani vurugu za polisi wa Tanzania dhidi ya Wamaasai” – Al Jazeera, 15 Juni 2022.
- “Tanzania: Ghasia zaidi zinahofiwa kwa jitihada za kuwafurusha Wamaasai kutoka kwa ardhi ya mababu” – UN News, 15 Juni 2022.
- “Mulika Afrika – Uondoaji wa Wamaasai wa Tanzania unaendelea” – BBC Sauti, 15 Juni 2022.
- “Tanzania yaanza kuwahamisha Wamaasai kutoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro” – France24/AFP, 16 Juni 2022).
- “Mapigano makali huku Wamaasai ‘wakitolewa ardhini’ kwa wawindaji wa nyara wa Imarati” – The Times, 18 Juni 2022
- “Mzozo wa Loliondo: Miaka 30 ya machungu na haki” (“Loliondo Conflict: 30 Years of Pain and Hope”) – BBC News Swahili, 18 Juni 2022
- “Mapigano ya Loliondo: Wamaasai wakitafuta msaada wa matibabu nchini Kenya” – BBC News, 21 Juni 2022.
Matamko ya mashirika na matamko mengineyo
Kufukuzwa huko Loliondo kulizua kilio cha kimataifa na kulaaniwa sana. Wataalamu mbalimbali wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya haki za binadamu na haki za ardhi, mashirika ya uhifadhi, taasisi za kitaaluma na watafiti, na watu mashuhuri wametoa taarifa, zikiwemo:
- Tume ya Afrika ya Haki za Kibinadamu na Watu: “Wito wa haraka wa kukomesha kufukuzwa kwa jamii ya Wamaasai katika wilaya ya Ngorongoro katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” (13 Juni 2022).
- Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Wenyeji: “Tamko la Mwenyekiti wa Jukwaa la Kudumu kuhusu kufukuzwa kwa Wamaasai kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro nchini Tanzania” (14 Juni 2022).
- Waandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa: “Tanzania: Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya kuongezeka kwa vurugu wakati wa mipango ya kuwaondoa kwa nguvu Wamaasai kutoka kwa ardhi ya mababu” (15 Juni 2022).
- Taasisi ya Oakland: “TAHADHARI YA HARAKA – Uwepo Mzito wa Polisi Loliondo kama Vitisho vya Kufukuzwa kwa Wamaasai Kuongezeka” (9 Juni 2022).
- Mpango wa Watu wa Misitu (ICCA Consortium Member): “Taarifa kwa Vyombo vya Habari: “Hatutaondoka. Sio kwa sasa. Si milele”: Taifa la Tanzania latwaa ardhi ya Wamaasai kwa nguvu huko Loliondo” (13 Juni 2022).
- Kikundi Kazi cha Kimataifa cha Masuala ya Wenyeji (IWGIA): “Tahadhari ya Haraka: Vitisho vipya vikali dhidi ya Wamaasai wa Loliondo nchini Tanzania” (13 Juni 2022) na “Hali ya Wamaasai huko Loliondo na Kuuzwa nchini Tanzania hatari na kukata tamaa” (05 Julai 2022).
- Amnesty International: “Tanzania: Sitisha operesheni ya kikatili ya usalama Loliondo” (15 Juni 2022).
- Muungano wa Kimataifa wa Ardhi: “Wamaasai wanafukuzwa kwa nguvu kutoka kwa ardhi yao” (15 Juni 2022).
- Frankfurt Zoological Society: “Tathmini ya hali ya Loliondo” (11 Juni 2022).
- Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN): “Tamko la IUCN kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu Loliondo, Tanzania” (19 Juni 2022) na “Tamko la ukiukwaji wa haki za binadamu katika uhifadhi” (28 Juni 2022).
- Uhifadhi wa Kimataifa: “Taarifa ya Kimataifa ya Uhifadhi kuhusu Ripoti za Unyanyasaji Dhidi ya Wenyeji Tanzania” (24 Juni 2022).
- Barua ya wazi: “Ukiukaji wa Umoja wa Afrika na Viwango vya Umoja wa Mataifa kuhusu Utawala wa Ardhi” – na Chuo Kikuu cha Western Cape, Taasisi ya Umaskini, Ardhi na Mafunzo ya Kilimo (16 Juni 2022).
- Makala ya maoni: “Afrika Mashariki lazima ikatae mtindo wake wa kikoloni wa kuhifadhi wanyamapori” – na mwandishi na mwanahabari wa kujitegemea Gatu wa Mbaria, iliyochapishwa na Guardian (24 Juni 2022).
- Makala ya maoni: “Kufukuzwa Loliondo: mbaya kwa watu, uhifadhi na ufugaji” – na watafiti Lucas Yamat na Pablo Manzano, iliyochapishwa na Pastres (24 Juni 2022).
- Barua ya wazi: “Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu sakata la Loliondo na Ngorongoro” – na Profesa Mstaafu Issa G. Shivji, Shule ya Sheria, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (25 Juni 2022).
Tafsiri kwa lugha la Kiswahili: Sharon Ruthia na Aquilas Koko Ngomo.